Mshambuliaji Emanuel Okwi leo ameanza kujifua na kikosi cha Simba mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Singida United keshokutwa.
Okwi amejiunga kikosi cha Simba mkoani Morogoro leo akitokea kwao nchini Uganda.
Akizungumza kuelekea mchezo dhidi ya Singida United, Okwi amesema Simba imedhamiria kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo licha ya ubora wa timu hiyo ya Singida.
"Mechi ijayo dhidi ya Singida sio nyepesi,tunawaheshimu na tunajua wana timu nzuri lakini Inshaallah tutapata matokeo mazuri.Dua na Sala zenu wanasimba wote," amesema Okwi

ADVERTISE HERE