Virusi vya Corona tayari vimeingia nchini, wananchi wametakiwa kujihadhari kwa kufuata taratibu za kujiepusha na maambukizi
Jinsi unavyoweza kujikinga
- Nawa vizuri na kila wakati mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20.
- Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.
- Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.
- Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
- Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimu
- Epuka kuwa sehemu yenye msongamano, kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.
- Nunua kifunika mdomo na pua na kukikavaa ukiwa kwenye mikusanyiko.
- Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.
ADVERTISE HERE