Klabu ya Simba iko kwenye mchakato wa kumsajili moja kwa moja kiungo mshambuliaji Deo Kanda ambaye alitua Msimbazi kwa mkopo akitokea klabu ya TP Mazembe
Mkataba wa mchezaji huyo na TP Mazembe unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na Simba ambayo imeonyesha nia ya kumsajili moja kwa moja
Taarifa za ndani zimeeleza kuwa Kanda mwenyewe anafurahia maisha kunako mabingwa hao wa nchi na amegoma kuongeza mkataba na Mazembe ambao wanafanya jitihada ya kumrudisha baada ya kuona kiwango chake kimepanda
Kanda ameifungia Simba mabao sita kwenye ligi na ni mmoja wa wachezaji ambao wanaaminiwa na kocha Sven Vandenbroeck
ADVERTISE HERE