Uongozi wa klabu ya Simba inakutana leo kujadili taratibu za kiusalama kwenye kambi ya timu hiyo katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona
Serikali imethibitisha kuingia kwa ugonjwa huo nchini ambapo jana Waziri Mkuu alitangaza kufunga shule zote kuanzia ngazi ya chekechea mpaka Sekondari kwa siku 30
Aidha Serikali pia ilitangaza kusitisha shughuli za michezo kwa siku 30
Ugonjwa huu ni janga kwa nchi nyingi ambapo barani Ulaya taarifa za wachezaji na viongozi kuambukizwa zimekuwa zikiripotiwa
ADVERTISE HERE