Kagere apewa na nafasi kuvunja rekodi ya miaka 21

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Mar 2020
Kagere apewa na nafasi kuvunja rekodi ya miaka 21

Mohammed Hussein 'Mmachinga' ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye msimu mmoja wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa na Yanga, mwaka 1999 aliweka rekodi ya kufunga mabao 26, rekodi ambayo hakuna mchezaji aliyeweza kuivunja mpaka leo

Hata hivyo Mmachinga amekiri  kutokana na kasi ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, anaweza kufikia rekodi hiyo iliyodumu kwa miaka 21

"Ingawa kasi yake ya kufunga inapanda na kushuka  ninampa asilimia 90, Kagere atafikisha rekodi niyoiweka na huenda akaivunja kwa sababu bado timu yake ina mechi nyingi za kucheza lakini pia anapewa nafasi kubwa ya kufunga  ndani ya Simba," alisema Mmachinga.

Kwa sasa Kagere anoongoza baada ya kufunga mabao 19 baada ya timu yake ya Simba kucheza michezo 28.

Msimu uliopita, Kagere alifunga mabao 23 na kutwaa tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

Msimu huu anahitaji kufunga mabao nane kutoka mechi 10 zilizobaki ili kuvunja rekodi hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
2h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
22h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’