Kuondoshwa kwa Simba kwenye michuano ya kombe la FA kisha michuano ya kombe la Mapinduzi, kulipelekea huzuni kubwa kwa mashabiki wa Simba kote duniani.
Kumekuwa na ukosoaji wa kila aina kuanzia benchi la ufundi mpaka kwa wachezaji.
Nahodha wa Simba John Bocco ametoa neno kuzungumzia hali hiyo.
Bocco amewataka mashabiki kutuliza presha na kuendelea kuwapa sapoti ili waweze kufanya kile ambacho wanakitarajia kutoka kwao.
Bocco amesema kuwa anatambua hawajafanya vizuri katika siku za karibuni hivyo wanapambana kurekebisha hali hiyo ili waweze kurudi kwenye ubora wao wakianzia na mechi za ligi ambayo inaendelea katikati ya wiki hii.
"Hata kama tumetolewa mapema kwenye kombe la FA na michuano ya Mapinduzi lakini sisi bado ni timu kubwa na yenye malengo ya ubingwa wa Tanzania Bara, hivyo sioni kwasababu gani mashabiki wetu wanakuwa wanyonge kwani tunaongoza ligi,"amesema Bocco.
Kwa sasa kikosi cha Simba kiko mkoani Morogoro kikijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Singida United utakaopigwa keshokutwa Alhamisi.
Aidha kurejea kikosini kwa kinara wa mabao Emanuel Okwi kumeongeza nguvu kwa kikosi hicho ambacho bado kinanolewa na Kaimu Kocha Masudi Djuma wakati mazungumzo juu ya kocha mpya yakiendelea.

ADVERTISE HERE