Bingwa Simba, mfungaji bora Kagere, imeisha hiyo...

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Mar 2020
Bingwa Simba, mfungaji bora Kagere, imeisha hiyo...

Ni suala la muda tu mabingwa wa nchi Simba wanarejesha ubingwa wao kwenye makabati ya pale Msimbazi kwa msimu wa tatu mfululizo

Ushindi katika mechi tano zijazo utaiwezesha Simba kumaliza msimu mapema tu wakiwa mabingwa pamoja na mechi zao tano mkononi

Huko kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu, nako ni kama mchele tayari umejitenga na chuya, Meddie Kagere anaongoza mbio akiwa amefunga mabao 19

Mabao nane zaidi ya wanaomfuata ambao ni Yusuf Mhilu (Kagera Sugar), Paul Nonga (Lipuli Fc) na Reliant Lusajo (Namungo Fc). hawa wote kila mmoja amefunga mabao 11

Huu utakuwa msimu wa pili mfululizo Kagere anaibuka mfungaji bora, msimu uliopita akitwaa kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao 23

Kazi aliyobaki nayo Kagere msimu huu ni kuhakikisha anavunja rekodi yake aliyoweka msimu uliopita

Ana mechi 10 za kufunga mabao matano ili kuvunja rekodi hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’