Sven awataka nyota Simba waonyeshe uwezo awape nafasi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Mar 2020
Sven awataka nyota Simba waonyeshe uwezo awape nafasi

Kumekuwa na maswali kutoka kwa mashabiki juu ya kutowaona baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha kwanza kwa muda mrefu

Hata hivyo Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema anatambua kuwa kikosi chake kimejaa wachezaji wenye vipaji lakini ni muhimu wakadhihirisha uwezo wao pale wanapopewa nafasi

Wadau wa Simba wamekuwa wakihoji alipo beki Yusufu Mlipili ambaye msimu huu hajaonekana kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuonekana katika mazoezi ya mabingwa hao wa nchi

"Nafahamu mashabiki wanapenda kuwaona baadhi ya wachezaji wakipata nafasi, hilo ni jambo jema kwani wachezaji wote tumewasajili kwa kuwa ni wazuri na tunataka waipe timu yetu mafanikio"

"Bahati mbaya katika mechi moja hatuwezi kutumia wachezaji zaidi ya 14, hivyo mara nyingi tunawapa nafasi wachezaji ambao wameonyesha utayari wa kucheza"

"Kila mchezaji ana nafasi sawa ya kucheza kama alivyo mwingine lakini ni muhimu akaonyesha mazoezini na anapopewa nafasi ya kucheza kuwa anastahili kuwemo kwenye kikosi cha kwanza," alisema Sven

Ukiondoa Miraji Athumani ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, nyota wengine ambao wamekuwa na nafasi finyu ya kuonekana kwenye kikosi cha Sven ni Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya, Gadiel Michael, Said Ndemla na Mzamiru Yassin ambaye mara ya mwisho alionekana dimbani kwenye mchezo wa kwanza wa watani wa jadi Januari 04 2020

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’