Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetangaza kusitisha kwa michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2021 ambayo ilikuwa ipigwe mwishoni mwa mwezi huu
CAF imechukua hatua hiyo baada ya Shirika la Afya Dunia (WHO) kutangaza kuwa maambukizi ya virusi vya Corona ni janga la dunia
Tanzania ilikuwa icheze na Tunisia mwishoni mwa mwezi huu na baadae mwezi April kushiriki michuano ya CHAN
Kuna uwezekano michuano ya CHAN nayo itaahirishwa
Wakati CAF ikichukua hatua hiyo, nyota wawili wa Simba Luis Miquissone na Sharaf Shiboub ameondoka leo kwenda kujiunga na timu za Taifa kwa ajili ya mechi hizo
Miquissone ameelekea Msumbiji kujiunga na timu ya Taifa hilo wakati Shiboub amekwenda kujiunga na Sudan
ADVERTISE HERE