Ukiondoa mechi kadhaa za viporo ambazo zinapigwa wikiendi hii, Ligi Kuu ya Vodacom imesimama kupisha mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia dhidi ya Tunisia ambao utapigwa mwishoni mwa mwezi huu
Lakini pia kuanzia April 05 mpaka April 19 fainali za michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani zitafanyika kule nchini Cameroon
Tanzania ni miongoni mwa mataifa 16 ambayo yatashiriki michuano hiyo
Hivyo ni wazi Ligi itasimama kwa zaidi ya mwezi mmoja kupisha michuano hiyo
Uongozi wa Simba unatarajia kutafuta mechi za kirafiki ili kuhakikisha kikosi kinaendelea kubaki katika hali ya ushindani kwani mapumziko hayo yanaweza kuwa na athari kwa timu kama wachezaji hawatapata michezo ya kirafiki ambayo itawapa ushindani
ADVERTISE HERE