Kisa cha kwanza cha virusi vya corona kimethibitishwa nchini Kenya. Waziri wa afya nchini humo Mutahi Kagwe amethibitisha kisa hicho katika tangazo alilolitoa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.
Bwana Mutahi amesema kwamba mtu mwenye maambikizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa ana maambukizi hayo Alhamisi usiku.
Waziri huyo amesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan nchini China.
Hii ni habari mbaya kwa Afrika Mashariki ambapo sasa ni lazima tahadhari zichukuliwe zaidi
Barani Ulaya maambukizi ya virusi vya Corona yamepelekea kwa mechi mbalimbali kusitishwa huku baadhi ya michezo ikichezwa bila ya mashabiki
Ligi za soka za nchi za Italia na Hispania zimesimamishwa huku baadhi ya mechi za ligi ya mabingwa na Europa zikipigwa bila ya mashabiki na nyingine zikisimamishwa
Ugonjwa huo umezidi kushika kasi huko Uingereza ambapo Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amebainika kuambukizwa. Pia winga wa Chelsea Callum Willson-Odoi nae amekutwa na maambukizi hali ambayo itapelekea mechi nyingi kusitishwa huku kukiwa na presha kubwa kutoka kwa wadau ambao wanataka mamlaka zisimamishe ligi hiyo pendwa duniani
Rais Magufuli ametoa tahadhari kwa wananchi kuchukua hadhari kwani ugonjwa huo ni hatari
''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.''
''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''.
''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga na tatizo hili''