jana Afisa Habari wa Simba Haji Manara ambaye yupo barani Ulaya alimkabidhi zawadi ya jezi ya Simba kiungo wa kimataifa wa Ureno ambae anachezea klabu ya Real Betis, William Carvalho.
Pia Manara alimpa zawadi ya jezi ya timu ya Taifa ya Tanzania kocha wa klabu hiyo Joan Francesc Sicilia maarufu kama Rubi

Pamoja na kuwa Manara amekwenda nchini Hispania kama balozi wa La Liga kutoka Tanzania, lakini ametumia fursa hiyo pia kuitangaza klabu yake pendwa ya Simba
Msemaji huyo wa Simba atafanya ziara kwenye mataifa mengine tisa ya Ulaya ambapo pamoja na mambo mengine, amesema atapata nafasi ya kukutana na Mawakala wa wachezaji ili kuwatengenezea mazingira wachezaji wa Kitanzania kupata fursa ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi
ADVERTISE HERE