Baada ya Yanga kutunguliwa bao 1-0 na KMC jana, kazi imezidi kuwa rahisi kwa mabingwa wa nchi Simba kutetea ubingwa wao kwa msimu wa tatu mfululizo
Kimahesabu Yanga wanaweza kufikisha alama 86 kama utatokea muujiza wakashinda mechi zao zote 12 zilizobaki
Hivyo Simba yenye alama 71 mpaka sasa, itahitaji alama 15 tu kuzifikia pointi hizo na alama moja zaidi ili kujihakikishia ubingwa
Pengine aama 15 zinaweza kutosha kutokana na wingi wa mabao ambayo Simba imefunga
Ikiwa imesalia na mechi 10, Simba inahitaji kushinda mechi tano tu
Katika mechi hizo, nne zitachezwa Dar na sita zitachezwa nje ya Dar
Mechi za nyumbani ni dhidi ya Ruvu Shooting, Alliance Fc, Mwadui Fc na Mbao Fc wakati mechi za mikoani ni dhidi ya Mbeya City, Tanzania Prisons, Ndanda, Polisi Tanzania, Namungo na Coastal Union