Mabingwa wa nchi Simba wametoa onyo kali kwa timu zinazoshiriki ligi kuu baada ya kuifumua Singida United mabao 8-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Kabla ya mchezo huo Mkurugenzi wa Singida United Festus Sanga alitamba kuwa timu yake ingeweza kuibuka na ushindi dhidi ya Simba leo
Hata hivyo balaa lililowakuta huenda wakasimulia kwa muda mrefu watakaporejea huko Singida
Ilikuwa siku nzuri kwa Meddie Kagere 'Terminator' aliyefunga mabao manne peke yake kwenmye mchezo huo
Kagere amefikisha mabao 19 na kuzidi kujichimbia kileleni kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Mabao mengine yalifungwa na Deo Kanda (2), John Bocco na Sharaff Elden Shiboub
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 71 sasa ikihitaji alama 18 tu itangaze ubingwa
Kabla ya mchezo, Mkufunzi wa Simba Sven Van denbroeck alikabidhiwa tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari
