Bosi Singida United atamba ataishangaza Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Mar 2020
Bosi Singida United atamba ataishangaza Simba

Licha ya kuwa ya mwisho mwenye msimamo wa ligi timu ya Singida United imepanga kuishangaza Simba kwa kuifunga katika mchezo wa ligi utakaopigwa uwanja wa Uhuru leo saa 10 jioni.

Simba itakuwa inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kukubali kipigo cha bao moja kutoka kwa watani wao Yanga siku ya Jumapili.

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Festo Sanga amesema kikosi chao kipo kamili na wana uhakika wa kupata matokeo ya ushindi mbele vinara hao wa ligi.

Sanga amesema katika mchezo wa leo hawatakuwa na kocha wao mkuu Ramadhani Nsanzurwimo ambaye hakusafiri na timu kutokana na kuugua.

"Kikosi kipo kamili na tuna uhakika wa kupata ushindi wa pointi tatu dhidi ya Simba. Tunataka ushindi tutakao upata tumpe pole kocha wetu ambaye anaumwa," alisema Sanga.

Kuhusu kuwa kwenye nafasi ya kushuka daraja kutokana na kuburuza mkia wakiwa na alama 12 pekee Sanga amesema hawawezi kushuka na wataanza kukusanya alama tatu leo kutoka kwa Simba

Wakati Sanga akitoa tambo hizo, Simba imepania kwelikweli kuifumua Singida United ili kupoza machungu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
44m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’