Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije leo ametangaza majina ya wachezaji 35 watakaounda kikosi cha awali cha timu hiyo kitakachocheza mchezo dhidi ya Tunisia baadae mwezi huu na fainali za michuano ya CHAN inayoshirikisha wachezaji wa ndani ambayo itafanyika mwezi ujao nchini Cameroon
Miongoni mwa wachezaji wa Simba waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni Aishi Manula, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Hassan Dilunga
Wengine ni John Bocco na Shomari Kapombe ambao wamerejeshwa kikosini baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na majeraha

ADVERTISE HERE