Sven kumaliza hasira kwa Singida United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Mar 2020
Sven kumaliza hasira kwa Singida United

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga hapo juzi

Sven ambaye ameiongoza Simba katika mechi zote mbili dhidi ya Yanga msimu huu na kuambulia alama moja, amesema anafahamu machungu waliyopata mashabiki lakini kama timu walipambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi

Amesema kikosi chake kiko tayari kuwapa furaha mashabiki kwenye mchezo unaofuta dhidi ya Singida United ambao utapigwa kesho Jumatano

"Ni matokeo yaliyotuumiza sisi sote, lakini nawaambia mashabiki wetu wasikate tamaa. Tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi kuliko wapinzani wetu lakini hatukuzitumia.

"Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya kosa moja wenzetu wakatuadhibu. Tumesahau matokeo hayo na sasa tunajipanga kwa mchezo unaofuata. Tunahitaji kushinda ili kuhakikisha tunatimiza lengo la kutwaa ubingwa," amesema Sven

Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 68 baada ya kushuka dimbani mara 27

Kimahesabu, inahitaji kushinda mechi saba kati ya 11 zilizobaki ili kujihakikishia ubingwa wa tatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’