DJuma atetea mfumo wake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
15 Jan 2018
DJuma atetea mfumo wake
Kocha wa Simba Madoud djuma amewaambia wanaokosoa mfumo wake anaoutumia wa sasa kwamba waache mazoea.

Wakosoaji hao wanadai kuwa mfumo unaotumiwa na kocha huyo umekuwa mgumu kwa baadhi ya wachezaji kwa mfano Shiza Kichuya ambaye mfumo huo unamfanya wakati mwingine kucheza akiwa na majukumu ya mlinzi wa kushoto wakati timu inashambuliwa.

“Watanzania waache mambo ya mazoea, mpira wa kileo kila mchezaji anakaba na kushambulia hakuna mpira ambao wachezaji wengine wanakaba wengine wanasubiri, mpira huo hakuna leo.”

“Angalia timu kubwa zote kila mchezaji anakuwa na majukumu sawa, kama uliangalia mechi ya Liverpoo na Manchester City utakuwa umeona kila mtu anakaba hakuna mchezaji ambaye hakabi uwanjani, ndio mpira wa kileo unakaba na kushambulia.”

“Ukiwa uwanjani kila mchezaji lazima ukabe usaidie wenzako, tukabe kama timu na kushambulia kama timu ndio mpira wa kisasa, mkitaka mpira wa kizamani wengine wanakaba huku wengine wanasubiri huo mpira haupo.”

Masoud ameiongoza simba katika mechi tano (moja ya ligi kuu, nne za Mapinduzi Cup) katika mechi hizo ameshinda mechi mbili moja ya ligi kuu (Ndanda 0-2 Simba) nyingine ya Mapinduzi Cup (Simba 3-1 Jamhuri) sare moja moja (Simba 1-1 Mwenge) huku akipoteza mechi mbili zote za Mapinduzi Cup (Simba 0-1 Azam, Simba 0-1 URA)
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7m ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →