Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewapongeza Yanga kwa kuweza kupata ushindi leo
Mo alikuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo ambao pia ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli
Mo amesema mpira ni furaha na utani, leo haikuwa siku ya bahati kwa Simba hivyo amewapongeza Yanga kwa ushindi
"Nawapongeza Yanga kwa ushindi Mungu awabariki, wamecheza vizuri. Mpira ni furaha na utani, nawapongeza," Mo aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo
Aidha Mo amesema kama timu watafanya tathmini ya mchezo huu ili kuweza kuboresha mapungufu yaliyojitokeza
"Masuala mengine hatutazungumza leo, kama Bodi na viongozi wa Simba tutafanya tathmini baadae, lakini leo hatuna wa kumlaumu"
ADVERTISE HERE