James Kotei pamoja na kuwa mbali na nchi, ametumia muda wake kuwahamasisha wachezaji na mashabiki wa Simba kuhakikisha ushindi unapatikana leo uwanja wa Taifa
Nyota huyo wa zamani wa Kaizer Chiefs, bado ni mwekundu kwelikweli kwani amekuwa akifuatialia kila kinachoendelea Msimbazi
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kotei amewapa wachezaji ujumbe wa hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa baadae leo uwanja wa Taifa
"Hii ndio mechi!Leteni furaha..wachezaji fanyeni mambo muwape furaha mashabiki wa Simba, Nguvu Moja...Nawatakia kila la kheri leo," aliandika Kotei
Kotei alishiriki mechi zote za dabi katika miaka mitatu ambayo alicheza Simba
Na rekodi yake ni kuwa hajawahi kupoteza mchezo wowote dhidi ya Yanga
ADVERTISE HERE