Hakuna shabiki wa Simba ambaye alifurahia matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04
Simba ilikuwa na kila sababu ya kushinda mchezo ule lakini uzembe wa hapa na pale ukapelekea Yanga wakarudisha mabao yote ndani ya dakika tatu
Uongozi wa Simba umesema mechi ya leo ni mwendelezo wa pale walipoishia kwenye mchezo wa kwanza
Pamoja na kuwa uhakika wa ubingwa kutua Msimbazi ni mkubwa, ushindi dhidi ya Yanga ni sherehe kubwa sana
Jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo', alitembelea kambi ya klabu hiyo na kuzungumza na wachezaji
Ujumbe wake ulikuwa mmoja, Wanasimba wanahitaji ushindi leo, matokeo tofauti na ushindi hayatakubalika hasa ikizingatiwa kilichotokea kwenye mchezo wa kwanza
Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kiko sawa, nyota wawili tu Said Ndemla na Miraji Athumani ndio majeruhi
Amewaahidi mashabiki kupata burudani ya kandanda safi ambayo itaambatana na ushindi