Tutacheza kama mabingwa - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Mar 2020
Tutacheza kama mabingwa - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga hawatakuwa na jingine zaidi ya kuhakikisha wanapata alama zote tatu na kujiweka mbele zaidi katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu

Akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo huo, Sven amesema vijana wake wako tayari kila mmoja akiahidi mchezo mzuri kuhakikisha wanapata ushindi

"Tutacheza mchezo huu kama sio mchezo wa Ligi sababu kila mmoja anajua tumewaacha kwa alama kadha"

"Tutaucheza kama mchezo wa kweli wa wapinzani kwahiyo tunajiandaa kuchukua alama tatu na kusonga mbele ili mwisho wa msimu tushinde, "amesema Sven

Nae nahodha wa mabingwa hao wa nchi John Bocco amesema hesabu zao ni kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu

"Sisi kama wachezaji tumejiadaa vizuri kwa mchezo wa kesho. Tunaahidi kwenda kucheza mchezo wa kujituma ili tuwafurahishe mashabiki wetu na ili tuweze kupata alama zote tatu"

Simba itaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa na kikosi chake kamili, Miraji na Ndemla ndio watakosekana kwa kuwa ni majeruhi

"Kwa upande wetu kila mmoja yupo fiti isipokuwa kwa Miraji na Ndemla ambao ni majeruhi. Nategemea hali nzuri kesho ambayo itaturuhusu kucheza mpira na kufurahia mchezo," amebainisha mkufunzi wa Simba, Sven

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’