Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' kesho Jumapili atakuwepo uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utaanza saa 11 jioni
Mchezo huo pia utashuhudiwa na Rais wa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad ambaye atakuwa mgeni wa heshima
Mo amewahamasisha mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa kumuonyesha rais huyo wa CAF ukubwa wa klabu ya Simba
Inaelezwa nyomi la mashabiki kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita ndio lililomsukuma Bw. Ahmad kuomba kuja nchini kushudua mbashara mchezo wa 'dabi'
ADVERTISE HERE