Sven awaandalia Yanga 'samba' la kutosha

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Mar 2020
Sven awaandalia Yanga 'samba' la kutosha

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Baada ya kuifumua Azam Fc mabao 3-2 Jumatano, Simba iliendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu

Sven amesema kuelekea mchezo huo hana mpango wa kufanya mabadiliko yoyote ya uchezaji kwa kikosi chake

Amesema mpaka sasa wamefanikiwa kupitia kandanda lao la pasi fupi fupi na anavutiwa na ushirikiano unaoonyeshwa na wachezaji wake

"Unajua Simba soka hili la pasi imekuwa kama ndiyo utamaduni wake, nimekuwa nikipenda kuona wachezaji wakicheza hivyo kwa sababu inasaidia zaidi timu kutengeza nafasi na ukiangalia tunapambania ubingwa, hatuhitaji kubadili kitu," amesema

Simba imejipanga kuondoka na alama zote tatu hapo kesho huku mashabiki wakija na msemo kuwa Yanga watasema walipataje sare ya mchezo wa kwanza uliopigwa Januari 04

"Kesho ndio watatujua Yanga, tunataka watuambie walipataje sare kwenye mchezo wa kwanza?," kauli ya Mama Simba, Mwanachama na shabiki kindakindaki wa mabingwa hao wa nchi

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’