FT : Azam Fc 2-3 Simba, salaam ziwafikie

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Mar 2020
FT : Azam Fc 2-3 Simba, salaam ziwafikie

Mabingwa wa nchi Simba leo wameendeleza wimbi la ushindi uwanja wa Taifa baada ya kuichapa Azam Fc mabao 3-2 katika mchezo mkali uliopigwa jioni ya leo

Simba iliuanza mchezo huo taratibu pengine hali hiyo ikichangiwa na timu kuchelewa kufika uwanjani kutokana na hali ya mvua

Waliwapa nafasi Azam Fc kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya tano likifungwa na Tigere

Hata hivyo kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Simba ambayo ilianza kupiga kandanda la kutisha na kufanikiwa kurudisha bao hilo dakika nne baadae mfungaji akiwa Erasto Nyoni

Kwenye dakika ya 16 Deo Kanda akaongeza bao la pili na kuiweka Simba mbele mpaka wakati wa mapumziko

Kipindi cha pili Azam walirejea na kasi walioanza nayo na wakafanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Iddi Selemani 'Nado'

Lakini bingwa ni bingwa tu, kwani Meddie Kagere 'MK14' aliihakikishia Simba ushindi muhimu kwa kufunga bao safi kwenye dakika ya 72

Matokeo haya yaliyoambatana na kandanda safi ni salamu kwa klabu ya Yanga ambayo siku ya Jumapili itakutana uso kwa uso na vijana wa Sven Vandenbroeck ambao wanauwasha moto kwelikweli

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’