Mshambuliaji wa Simba kinara wa mabao ligi kuu Meddie Kagere huenda akarejea kikosini baadae leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Taifa
Kagere alipumzishwa mchezo uliopita dhidi ya KMC kwa kile kilichoelezwa kuugua ghafla
Hata hivyo nyota huyo anayeongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akifunga mabao 14, yuko sawa tayari kwa mchezo wa leo
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema Kagere anaweza kuwemo kwenye kikosi kitakachoikabili Azam Fc leo kama kocha Sven Vandenbroeck ataamua kumtumia
Kagere ndiye aliyafunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa duru ya kwanza dhidi ya Azam Fc
ADVERTISE HERE