Azam Fc vs Simba, mechi ya kibabe uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Mar 2020
Azam Fc vs Simba, mechi ya kibabe uwanja wa Taifa leo

Mabingwa wa nchi Simba leo wanatupa karata muhimu uwanja wa Taifa watakapoikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku

Ugumu wa mchezo huo unatokana na ubora wa timu ya Azam kwani ukiondoa Simba pengine Azam Fc na kidogo Yanga ndio zinazofuata kwa ubora miongoni mwa timu zinazoshiriki ligi kuu

Lakini pia msimu huu tayari Azam Fc imeshakubali vipigo viwili kutoka kwa Simba

Kipigo cha kwanza kilikuwa cha mabao 4-2 mchezo wa Ngao ya Jamii kisha kupigwa bao 1-0 mchezo wa duru ya kwanza ligi kuu

Hivyo ni wazi wataingia kwenye mchezo huo kujaribu kujihami na kipigi cha tatu mfululizo

Hata hivyo wanakutana na Simba wakati mbaya, kwani mabingwa hao watetezi wamerejea kwenye ubora wao

Simba imeshinda mechi tano mfululizo kwenye ligi na sasa inapiga hesabu za kutwaa ubingwa mapema

Ushindi katika mechi nane kati ya 13 zilizobaki, utaihakikishia Simba kutwaa ubingwa

Mkufunzi wa timu hiyo Sven Vandenbroeck amesema ushindi katika mechi ya leo na inayofuata dhidi ya Yanga ndio matokeo muhimu zaidi kwao kuelekea kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’