Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema wanachama na mashabiki wenye mapenzi mema walifika ofisini kwake mapema leo na kumkabidhi fedha Tsh Milioni Moja ili azirudishe kwa Yanga ambao walimchangia wakati akiumwa macho
Manara amesema atazirudisha fedha hizo baada ya aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga Jerry Muro (DC) kuendelea 'kumsimanga' kwa kuwa alifanikisha kupatikana kwa fedha hizo miaka kadhaa iliyopita
"Washabiki wa Simba wamenijia ghafla leo ofisini na kunikabidhi shilingi milioni moja ambazo zilichangwa kwa hiyari na Group moja la Watsap la Yanga wakati nilipoumwa macho,ili pesa hizo nizirejeshe baada ya baadhi ya Wanayanga kuendeleza masimango eti wao ndio walinitibia india"
"Kiukweli inaumiza sana kurejesha pesa lakini inaumiza sana pale mmoja katika wasemaji wao anaposema yeye ndio alinitibia"
"Nimezipokea pesa hzo na naendelea kumtafuta Bumbuli ili nimkabidhi mchango wao waliotoa kwa hiyari yao.. Shukran Wanasimba kwa kujali," amesema Manara


Hata hivyo Manara alisitisha mpango wa kurudisha fedha hizo baada ya mashauriano ya Wazee wa klabu ya Yanga aliowakuta Makao Mkuu ya klabu hiyo mchana wa leo
Manara amepanga kuziwasilisha fedha hizo kwa makundi yenye uhitaji