Simba yapiga hesabu za Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Mar 2020
Simba yapiga hesabu za Ligi ya Mabingwa

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amesema timu hiyo inajipanga kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika itakayoanza mwezi August mwaka huu

Baada ya Simba kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa, tayari kocha mkuu wa timu Sven Vandenbroeck ameweka mezani mapendekezo yake ya usajili

Inaelezwa Mbelgiji huyo tayari ameuweka sawa uongozi wa Simba uandae bajeti ya kutosha ili kuweza kusajili wachezaji watakaokuwa na mchango mkubwa kwenye michuano hiyo

"Kuna maeneo ambayo kocha ametuambia na tayari tumeanza kuwafuatilia wachezaji ambao watakuja ni wenye vigezo vya kucheza Simba, tutaangalia bajeti yetu ili kuweza kusajili wachezaji wanaoendana na hadhi ya Simba kwa kutoka kila pembe ya Afrika," amesema Senzo

Aidha Senzo amesema msimu ujao wamejipanga kuhakikisha wanaunda kikosi imara ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo

"Kutolewa mapema kwenye michuano ya mwaka huu lilikuwa somo kwetu, hatutarudia makosa. Tumejipanga kuimarisha kikosi chetu kwa kuongeza wachezaji ambao watatusaidia kufanya vizuri"

Miongoni mwa maeneo ambayo yanatarajiwa kufanyiwa maboresho ni eneo la safu ya ulinzi ambalo kwa sasa linawategemea zaidi wakongwe Paschal Wawa na Erasto Nyoni

Hata hivyo mabeki hao umri umewatupa mkono hivyo kuwepo kwa ulazima wa kuongeza nguvu hasa baada ya nyota wengine waliosajiliwa kwenye nafasi zao kushindwa kufikia matarajio

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’