Azam Fc kwanza, Yanga baadae - Bocco

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Mar 2020
Azam Fc kwanza, Yanga baadae - Bocco

Nahodha wa Simba John Bocco amesema baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, sasa wanaelekeza nguvu zao kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc

Bocco jana aliongoza safu ya ushambuliaji akishirikiana na Luis Miquissone baada ya Meddie Kagere kuugua. Amesema kwa sasa hawaufikirii mchezo dhidi ya Yanga kwani wanahitaji kumalizana na Azam Fc kwanza

"Ushindi tunaopata unatuongezea hali ya kujiamini kuelekea mechi zetu dhidi ya Azam na Yanga. Tuna siku mbili za kujiandaa kabla ya kukutana na Azam na ndio mechi tunayo iangalia kwa sasa kabla ya kukutana na Yanga," amesema Bocco

Mchezo dhidi ya Azam Fc utapigwa keshokutwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa wakati ule dhidi ya Yanga utapigwa Jumapili

Bocco amerejesha makali yake baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa zaidi ya miezi mitatu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’