Bado mashabiki wa Simba wana shauku ya kumuona beki Yusufu Mlipili akipata nafasi ya kucheza msimu huu
Kwani tangu kuanza kwa msimu, beki huyo aliyafanya vizuri msimu uliopita, hajaonekana kikosini
Kocha Sven Vandenbroeck anawatumia Erasto Nyoni na Paschal Wawa na wakati mwingine akiwapa nafasi Tairone Da Silva na Kenedy Juma
Hata hivyo viwango vinavyoonyeshwa na Tairone na Kenedy vinawapa wasiwasi mashabiki ambao wanadhani ingekuwa vyema kumjaribu Mlipili hasa Wawa au Nyoni anapokosekana
Hata hivyo maamuzi ya mwisho yanabaki kwa Vandenbroeck ambaye ndiye anafahamu viwango vya wachezaji wake na jinsi ya kuwatumia kulingana na mechi husika
ADVERTISE HERE