Simba wanataka kutwaa ubingwa wa mataji yote kwa kishindo kwa imani kwamba jambo hilo litaweka heshima kubwa kwao katika soka la Tanzania.
Nyota wa timu hiyo wanataka kushinda mechi zote ngumu kwa kuanzia hii ya Machi 8 dhidi ya Yanga
Kiungo wa Wekundu wa Msimbazi, Jonas Mkude amesema anajua kwamba kabla ya kuwafikia Yanga, mbele yao kuna mechi mbili ya Namungo na Azam FC na kwamba zote hizo nyota wa Simba wamedhamiria kutoa vipigio vikali
Anaamini kwamba wakishinda hizo zitawapa morali zaidi ya kupambana ili kufikia malengo yao
"Ingawa kwa mchezaji hakuna mechi rahisi lakini kuna zile ambazo mashabiki wanakuwa na shaka, hizo ndizo tunazotamani kushinda kwa kishindo ili tukitetea ubingwa iwe kwa kishindo," alisema Mkude
"Sio kazi rahisi lakini naamini kila mchezaji akituliza akili yake kila kitu kitafanyika kwa mafanikio ya hali ya juu"
Nje na mechi ya KMC, Azam na Yanga pia alisema anatamani kuona wanavuna pointi sita mkoani Mbeya dhidi ya Prisons na Mbeya City ambako mtu ukishinda unaona fahari kutokana na ugumu wake