Sven ataka alama 12 kutoka mechi nne zijazo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Feb 2020
Sven ataka alama 12 kutoka mechi nne zijazo

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck tayari ameshaona ubingwa wa tatu mfululizo unanukia Msimbazi na sasa anataka kuuweka kibindoni mapema zaidi

Kesho Sven ataiongoza Simba kuikabili KMC katika mchezo utakaopigwa saa mbili usiku uwanja wa Taifa

Ni mchezo ambao Mbelgiji huyo amesema wanahitaji kusepa na alama zote tatu pia washinde michezo mingine itakayofuata kabla ya ligi kusimama March 18

"Tunafahamu ligi itasimama March 18 kuipa nafasi timu ya Taifa kwenda kushiriki michuano ya CHAN, tutacheza mechi tatu hadi nne. Tunahitaji kushinda mechi zote ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa"

"Tunahitaji kupata matokeo kuanzia mchezo dhidi ya KMC. Tumefanya maandalizi ya kutosha na tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri. Mashabiki waje kwa wingi wapate burudani," amesema

Miongoni mwa michezo ambayo Simba itacheza wiki ijayo ni dhidi ya Azam Fc na Yanga. Ushindi katika mechi hizi utaisogeza Simba karibu zaidi ya ubingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
7h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’