Wakati mchezo wa watani wa jadi ukiwa karibu, hatma ya kiungo fundi Jonas Mkude inasubiri kikao cha Kamati ya Nidhamu ya TFF
Mkude alipelekwa mbele ya Kamati hiyo kufuatia tukio la kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United wiki iliyopita katika mchezo ambao Simba ilishinda mabao 3-1
Bado Kamati hiyo haijakutana lakini kuna uwezekano wa nyota huyo pamoja na Bernard Morrisson wa Yanga wakakosa mchezo huo kutokana na kesi zinazowakabili
Wakati akisubiri hatma yake, Mkude anaruhusiwa kuendelea kuitumikia Simba mpaka pale Kamati hiyo itakapokutana na kutoa maamuzi
ADVERTISE HERE