Michezo ya raundi ya tano michuano ya kombe la FA (ASFC) imekamilika leo kwa miamba nane iliyotinga robo fainali kufahamika
Matokeo ya michezo iliyopigwa leo yameziwezesha timu za Azam Fc, Kagera Sugar, Alliance Fc na Yanga kupenye robo fainali
Timu hizo zimeungana na Simba, Namungo Fc, Ndanda Fc na Sahare All Stars timu pekee iliyobaki kutoka ligi daraja la kwanza
Kinachosubiriwa sasa ni droo ya hatua ya robo fainali
Mchezo wa fainali mwaka huu utapigwa May 30 mkoani Rukwa uwanja wa Nelson Mandela
ADVERTISE HERE