Afisa Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amemjibu Jerry Muro aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Muro ambaye jana alitangaza kurejea Yanga kwa kile alichodai kuongeza hamasa kuelekea mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa March 08, alihoji kwa nini Manara amekuwa Msemaji wa Simba kwa muda mrefu
Manara amesema tofauti ya yeye (Muro) wakati akiwa Yanga, Simba ni ajira yake, anapendwa na mashabiki na anaaminiwa na viongozi hivyo hana sababu ya kuacha ajira yake
"Unahoji kwa nini Haji haondoki jamani hii si ajira yake kwanini aondoke? kwahiyo niache kazi Simba napendwa wanasimba wanaridhika na kazi yangu wewe unataka niondoke si roho mbaya ya wazi," alisema Manara
"Kwanza kwa kauli yake hiyo, imenifanya nianze kuhofia usalama wangu"
"Siwezi kutembea peke yangu wanaSimba wanilinde Serikali inilinde naweza kupigwa hata risasi kama wamefika mahali wanataka niondoke wanaweza kuniua hawa," alisema Manara
Kwa miaka ya hivi karibuni Manara amekuwa kinara wa kuitangaza chapa ya Simba jambo lililomuongezea umaarufu
Yanga pamoja na kuwa na wasemaji wawili (Muro akiwa wa tatu) bado wameshindwa kufua dafu dhidi yake