Saa mbili na robo usiku mabingwa watetezi wa michuano ya michuano ya kombe la Mapinduzi, Azam FC watashuka kwenye dimba la Amani kujaribu kutwaa taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo watakapowavaa watoza ushuru wa Uganda, URA.
Michuano hiyo iliyoanza Disembe 29, 2017 inafika tamati leo kwa mchezo huo wa fainali.
Azam FC na URA zinakutana kwa mara ya pili kwenye michuano hiyo kwani zilikuwa kundi moja, A.
Katika hatua ya makundi URA iliichapa Azam FC bao 1-0 na hivyo kuufanya mchezo huo uwe wa kisasi kwa Azam FC.
Wakati michuano hiyo ikifikia tamati leo, wadau wa soka wameshauri michuano ijayo ifanyiwe marakebisho katika upangaji wa ratiba
Wamekosoa ratiba inayolazimu kucheza mechi mfululizo kwani si jambo zuri kwa wachezaji kiafya.

ADVERTISE HERE