Simba imefanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali kombe la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya Stand United
Mshindi wa mchezo alilazimika kupatikana kwa changamoto ya penati baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1
Hassan Dilunga aliitanguliza Simba kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 52 baada ya mlinzi wa Stand kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari
Stand wakarejea mchezoni kwa bao la kusawazisha dakika ya 67 lililofungwa na Miraji Saleh
Pamoja na changamoto ya uwanja, Simba imepata ushindi muhimu ambao umewapeleka hatua inayofuata wakiungana na Namungo, Ndanda Fc na Sahare All Stars
ADVERTISE HERE