Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wachezaji wake 29 wako tayari kwa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Stand United ambao utapigwa kwenye uwanja wa Kambarage leo Jumanne, Februari 25 2020
Hata hivyo Sven amesema sio wachezaji wote watapata nafasi ya kucheza lakini anatarajia kufanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kuwapa nafasi nyota wengine
"Kila mmoja yupo tayari kwa mchezo lakini kwenye mchezo mmoja hatuwezi kutumia wachezaji wote 29 hivyo lazima kuchagua wachezaji wa kuwatumia, na kwa huu mchezo labda kutakuwa na mabadiliko machache," amesema
Aidha Sven amewataka mashabiki wa Simba mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa vinara hao wa ligi kuu
"Mashabiki wetu wajitokeze kutushangilia, tupo kwenye hali nzuri na kesho tutacheza mchezo mzuri"