Dalali awataka wachezaji wajitambue

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
13 Jan 2018
Dalali awataka wachezaji wajitambue
Mwenyekiti wa zamani wa Simba Mzee Hassani Dalali amewashukia wachezaji mastaa wa klabu hiyo kwamba wanatakiwa kujituma na kupambana kwa ajili ya klabu ili ipate ubingwa, hakuna mchezaji ambaye ni mkubwa kuliko klabu ndio maana wamesajiliwa.

Dalali amsema hakuna kitu kingine ambacho wanachama wa klabu hiyo wanahitaji zaidi ya ubingwa ambao wameukosa kwa muda mrefu.

“Hata kama jina lako kubwa Simba ni kubwa kuliko wewe ndio maana imekusajili, onesha uwezo wako sisi tunahitaji ubingwa hakuna kitu kingine.

"Katika miaka nane tangu nimeondoka madarakani tumechukuwa ubingwa mara moja (2011/12) wakati Ismail Aden Rage akiwa madarakani lakini ubingwa ule si kwa kumfunga mtu, wamecheza Mtibwa na Azam, kafungwa Azam Simba kawa bingwa wakati yupo nyumbani kalala.”

“Timu ya Mbao kuna kijana mdogo anaitwa Imran Kalman ameidhamini Mbao kawapa basi anatoa pesa nyingi katika timu, angalia Mbao wanavyocheza wanajituma, wanaona thamani ya timu yao walicheza na Simba 2-2 Yanga kaingia kafungwa iweje sisi Simba?

"Wachezaji wanashindwaje kupafomu uwanjani? Wanachama wanaumia, mimi naomba wachezaji wa Simba kama kuna tatizo waweke wazi kwa viongozi, wazee au wadhamini wa klabu wakaseme kama wanadai au viongozi.”
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →