Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Biashara United, mabingwa wa nchi Simba wameondoka Alfajiri ya leo kuelekea mkoani Shinyanga tayari kwa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Stand United
Tayari vinara hao wa ligi kuu wamewasili mkoani Mwanza ambako watachukua usafiri wa basi kuelekea Shinyanga
Simba itakuwa mgeni wa Stand United katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa CCM Kambarage keshokutwa Jumanne, Februari 25 2020


ADVERTISE HERE