FT : Simba 3-1 Biashara United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Feb 2020
FT : Simba 3-1 Biashara United

Mabingwa wa nchi Simba wameendelea kuusogelea ubingwa wa tatu wa ligi kuu baada ya kuichapa Biashara United mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Luis Miquissone kwa mara nyingine leo aliteka 'shoo' akiifungia Simba bao la kuongoza kwa shuti kali kwenye dakika ya 35 muda mfupi baada ya Meddie kagere kukosa mkwaju wa penati

Simba iliyokuwa ikicheza 'sexy football', iliwapoteza kabisa wapinzani wao Biashara United ambao muda mwingi walikuwa wakiutafuta mpira kwa tochi

Bao la pili lilipatikana kwenye dakika ya 68 mfungaji akiwa Meddie Kagere ambaye alifanya kazi rahisi ya kuusukumiza mpira wavuni baada ya krosi murua iliyochongwa na Miquissone

Biashara United walitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba kupata bao la kufutia machozi kwenye dakika ya 71

Lakini Simba ilimaliza mchezo huo kibabe kwa kufunga bao la tatu kwenye dakika ya 88 kupitia kwa Francis Kahata

Kabla ya kuingia bao hilo zilipigwa pasi kadhaa kama vile wafanyavyo vijana wa Klopp kule Uingereza

Simba imefikisha alama 62 sasa ikiongoza kwa tofauti ya alama 17

Pengine shamrashamra za ubingwa wa ligi kuu zitafanyika mapema tu msimu huu pale Msimbazi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’