Pamoja na Biashara United kuwa kwenye kiwango bora, Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema wamejipanga kuwapa furaha mashabiki wao kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo utakaopigigwa baadae leo Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Biashara United haijafungwa katika michezo sita iliyopita, wakishinda michezo minne na kutoka sare michezo miwili
Sven amesema wanatambua wapinzani wao kuwa na mwenendo mzuri lakini wamejiandaa kuondoka na alama zote tatu uwanja wa Taifa
"Biashara ina rekodi nzuri, haijapoteza tangu ilipofungwa na Yanga. Ipo kwenye kiwango bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo kwa kucheza soka safi," amesema Sven akizungumzia maandalizi ya kikosi chake
Simba itaingia kwenye mchezo huo ambao utapigwa saa moja jioni ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza uliopigwa Musoma mwishoni mwa mwaka jana