Okwi, Niyonzima bado hakieleweki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
13 Jan 2018
Okwi, Niyonzima bado hakieleweki
Hali bado si shwari sana ndani ya kikosi cha Simba baada ya wachezaji wake Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima kushindwa kufanya mazoezi na timu hiyo inayojiandaa na mechi dhidi ya Singida United.

Simba inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Bandari Temeke chini ya kocha Masoud Djuma mwenye lengo la kushinda mechi yake dhidi ya Singida United ili kurudisha amani na imani ndani ya klabu hiyo baada ya kufanya vibaya katika Kombe la Mapinduzi.

Niyonzima na Okwi walikosekana katika kikosi cha Simba kilichoshiriki mashindano ya Mapinduzi na kuambulia kutolewa katika hatua ya makundi.

Okwi amekuwa nje ya kikosi hicho kwa muda mrefu kutokana na kuwepo kwa madai kuwa anamahitaji yake binafsi bado hajatimiziwa na uongozi wa Simba.

Suala la Okwi limeonekana kuwa juu ya kocha Djuma kwani hata viongozi wa Simba wameshindwa kuweka wazi kwani mchezaji huyo ameshindwa kuungana na kikosi hicho kwa zaidi ya mwezi sasa.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba, Hans Poppe alisema taarifa alizonazo Okwi bado anaendelea na matibu na si vinginevyo kama baadhi ya watu wanavyosema anadai fedha zake za usajili.

“Nilivyopata habari Okwi ni kwamba alikuwa anauguza shingo huko kwao sasa kama hayupo ni kwa sababu ya kuumwa”-Hans Poppe.

Naye Niyonzima alisema bado hajapona na anaendelea mazoezi kidogo kidogo huku akiwa chini ya uangalizi wa daktari wake ndio atampa ruksa ya kurudi uwanjani.

"Nafanya mazoezi mwenyewe sijasikia uwezo wa kufanya na timu kwani bado sijawa fiti kiasi kikubwa ndio maana nafanya mazoezi yangu madogo chini ya uangalizi, " alisema kiungo huyo.

"Kuhusu kuwepo kwenye mechi dhidi ya Singida United, sijajua kwani maendeleao yangu yanaendelea kuwa vizuri, lakini taratibu taratibu na kama daktari ataniruhusu sawa nitarudi uwanjani, lakini kama nitakuwa bado basi nitaendelea na mazoezi, " alisema Niyonzima.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
13h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
14h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →