Msimu huu tunataka heshima - Mkude

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Feb 2020
Msimu huu tunataka heshima - Mkude

Kiungo Jonas Mkude amesema kiu yake na wachezaji wenzake wa Simba ni kuona wanamaliza msimu kwa heshima kwa kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo

Mchezaji huyo mwandimizi ndani ya Simba amesema pointi walizonazo na mechi zilizosalia kwao ni nafasi ya kupambana kuziongeza ili kuchukua taji mapema kabla ligi9 haijaisha na hiyo itakuwa heshima kwao.

"Ligi ni ngumu unapokuwa kileleni inakupa nguvu ya kuongeza juhudi zaidi ukijua kuna timu inayotamani kuwaondoa ndio maana ya kuwania taji la ligi kuu," alisema Mkude aliyeifungia mabao moja katika msimu huu na kuongeza;

"Tunatamani kumaliza ligi kibabe, japo tunatambua kwamba si kazi rahisi kwani tunakwenda kucheza na timu zinazojikwamua kushuka daraja, hivyo zitakuwa mechi za kisasi."

Mkude amesema wanatamani kuandika rekodi ya kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo ili kutimiza lengo lao na kuweka heshima mbele ya mashabiki wa Simba na wale wa soka la Tanzania kwa ujumla.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’