Nahodha wa Simba John Bocco sasa yuko imara baada ya kuanza mechi tatu mfululizo na moja kwa moja kuhusika katika ushindi
Katika mechi hizo Bocco amefunga mabao mawili, ametoa pasi moja ya bao na pia kusababisha mkwaju wa penati kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Meddie Kagere aliweka kambani penati hiyo na kufunga bao lake la 13 msimu huu
Bocco hakuanza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga Januari 04 ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2
Lakini bila shaka, March 08 ataongoza safu ya ushambuliaji sambamba na pacha wake Kagere 'MK-14'
Majeraha yalimuweka nje kwa muda mrefu nahodha huyo wa mabingwa wa nchi kabla ya kurejea dimbani mwishoni mwa mwaka jana
ADVERTISE HERE