Bao la mkwaju wa penati alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, limemfanya mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere afikishe mabao 13 na kujiimarisha kileleni katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu
Mabadiliko ya benchi la ufundi Simba yalionekana kumpunguza Kagere kasi ya kufunga lakini bao lake la jana limemrejesha kwenye utamaduni wake wa kucheka na nyavu
Reliants Lusajo wa Namungo Fc na Yusuf Mhilu wa Kagera Sugar wanamfuatia kwa mbali wakiwa wamefunga mabao tisa kila mmoja
Daruweshi Saliboko wa Lipuli Fc pamoja na Obrey Chirwa wa Azam Fc wao wamefunga mabao nane kila mmoja
Bigirimana Blaise (Namungo), David Molinga (Yanga), Peter Mapunda (Mbeya City) na Paul Nonga (Lipuli) wao wamefunga mabao saba kila mmoja
Hassan Dilunga na Miraji Athumani wa Simba, wanaunga na Adam Adam wa JKT Tanzania na Ayoub Lyanga wa Coastal Union wakifunga mabao sita kila mmoja