Pluijm apania mchezo dhidi ya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
12 Jan 2018
Pluijm apania mchezo dhidi ya Simba
Kocha Mkuu wa Singida United Hans Van Pluijm amefichua kuwa baada ya kuondoshwa kwenye kombe la Mapinduzi, akili zake sasa ni kwenye mchezo unaokuja dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba.

Pluijm alisema mashindano ya Mapinduzi yalikuwa mazuri na anajivunia kiwango ambacho wachezaji wake wameonyesha licha ya kuwa ndio mara yao ya kwanza kushiriki. Singida ilifungwa bao 1-0 na Azam kwenye mchezo wa nusu fainali.

“Mashindano ni mazuri na kufika katika hatua ya nusu fainali ni kitu kikubwa kwetu kwani inaonyesha jinsi gani tunazidi kuimarika, tumeyachukua pia mashindano haya kama maandalizi ya mechi za ligi kuu,” alisema Pluijm.

“Changamoto ambayo ilikuwa kwetu ni kucheza mechi nyingi kwa kipindi kifupi jambo ambalo lilikuwa linapunguza uwezo wa wachezaji wangu," alisisitiza.

“Tunacheza mechi ijayo na Simba katika ligi, ni timu ngumu yenye wachezaji wazuri, tunaanza maandalizi mapema ili kupata matokeo ya ushindi," alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →