Baada ya kipigo cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa duru ya kwanza, Mkufunzi wa Kagera Sugar Meckie Mexime amesema kesho wataikabili Simba kwa tahadhari kubwa
Msimu uliopita Kagera Sugar ilipata ushindi kwenye michezo yote miwili dhidi ya Simba matokeo ambao yaliwafanya watoe tambo nyingi kuelekea mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa Bukoba Septemba 26 2019
Mexime amesema anafahamu anakwenda kukutana na Simba iliyo imara hivyo wanapaswa kujihadhari
Kesho Simba inarejea kucheza uwanja wa Taifa baada ya kushinda mechi zake mbili zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar mkoani Morogoro na Lipuli mkoani Iringa
Mabingwa hao wa nchi hawakuruhusu bao katika michezo yote miwili baada ya kocha Sven Vandenbroeck kumrejesha langoni Aishi Manula maarufu 'Tanzania One'
Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utapigwa kuanzia saa moja usiku uwanja wa Taifa