Ule mjadala kuwa ni timu gani yenye mashabiki wengi hapa Tanzania kati ya Simba na Yanga kwa sasa huwezi kuusikia tena kwani Simba imedhihirisha kuwa ndio baba wa soka la Tanzania
Ndio timu inayoungwa mkono zaidi, sio ndani ya nchi pekee pengine hata ukanda wa Afrika Mashariki na kati
Achana na utamaduni wa kujaza uwanja wa Taifa kwa mechi zote kubwa ambazo Simba inacheza, lakini mabingwa hao wa nchi wanapokwenda mikoani, wanapata uungwaji mkono usio wa kawaida
Simba inajivunia kuwa na mashabiki 'wafia timu' ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio yanayoendelea kupatikana



ADVERTISE HERE